MAISHA YAMEBADILIKA,THAMANI YA MWANAMKE NI KUJITEGEMEA KIUCHUMI

0

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Roijo Progress Center ikishirikiana na serikali, wamezindua siku ya batiki Tanzania ambayo inalenga kufungua fursa za uuzaji wa batiki hizo ndani na nje ya nchi.




Uzinduzi wa siku hiyo ya batiki ulifanyika katika maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam(DITF), yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Rose Urio, amesema lengo lake ni kuitangaza batiki katika soko ndani na nje ya nchi pamoja na kumpatia mwanamke kuitumia fursa hiyo kujiingizia kipato.

 ​​​​“Tunafahamu kwamba batiki ni fursa ya kibiashara ambayo inafanywa na mtu yeyote, lakini hapa tunataka mwakamke ndiye aichangamkie zaidi ili imsiadie kujikwamua kiuchumi,”amesema Rose.

“Miasha yamebadilika, thamani ya mwanamke ni kujitegemea kiuchumi, batiki ni bidhaa ambayo inaweza kuzalishwa hata katika eneo dogo lenye uwazi, kwa hiyo tunawahamasisha wanawake waingie kwenye fursa hii,”amesema Rose.

 Amesema katika mradi huo wa batiki, wanatarajia kuzinda ua maalum linalojulikana kama ‘ua la mama’ ambalo lengo lake litakuwa ni kumuenzi Rais wa sasa, Samia Suluhu Hassan.

“Na tumejipanga kuhakikisha kwamba tunaboresha zaidi batiki zetu.Mpaka sasa hatuna standard za batiki zinazofanana, tunazozizalisha sasa ni zile ambazo unakuta mmoja na mita mbili na nusu, mwingine tatu au nne kabisa, kwa hiyo tunataka tupate standard moja,”amesema Rose.

Amesema kupatikana kwa viwango vya bidhaa hiyo, itasaidia kuviuza na kushindana katika soko la ndani na nje ya nchi.

TAZAMA VIDEO HII YA WAHAMIAJI HARAMU WAKIHUKUMIWA KWENDA JELA MAKETE


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top