Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Joyce Mkazi wa mtaa wa Misunkumilo Manispaa ya Mpanda Mkoani katavi amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya chumba chake cha kulala.
Akizungumzia tukio hilo mmewe na marehemu amesema hajui sababu iliyopelekea Mkewe kuchukua hatua hiyo ngumu ambayo imepelekea yeye kujinyonga na kumuacha mtoto mdogo anaye nyonya.
Kwa upande wao majirani wa eneo hilo wamesema kulikuwa na migogora kati yake na mke mwenza wenda ikawa chanzo cha yeye kuchukua maamuzi ya kujitoa uhai wake.
Diwani wa kata Misunkumilo Matondo pamoja na mjumbe wa serikali ya mtaa wa Misunkumilo wamesema wamepewa taarifa za mtu kujinyonga na wamefika eneo la tukio lakini hawajawa na taarifa iliyopelekea Joyce kujinyonga.
Jeshi la Polisi limefika eneo la Tukio ili kufanya uchunguzi Wa tukio hilo na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadae!