Wanafunzi 35 wa waliofaulu kidato cha nne mwaka 2022 katoka skuli tano za jimbo la Chambani wametakiwa kuongeza bidii katika masomo yao ili kuendelea kufanya vizuri katika mitahani ya kidato cha sita.
Akitoa zawadi ya mikoba, madaftari
pamoja na sare kwa wanafunzi hao Mbunge wa jimbo wa la Chambani Mhe. Mohammed
Abrahmani Mwinyi, amesema uongozi wa jimbo hilo umejitolea kwa dhati kuisaidia
sekta ya elimu ili kuhakikisha wanafunzi wa jimbo hilo wanafanya vizuri katika
masomo yao.
Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwakushirikiana na Serikali ya jamhuri ya Tanzania zimetoa fursa ya elimu bure kuanzia elimu ya darasa la saba hadi kidato cha sita ili kuhakikisha kila raia anapata haki ya msingi ya elimu.
“Munatoka hapa munakwenda hatua
nyengine nawaomba acheni utoto 2024 tuhakikishe hakuna mwanafunzi aliyepata division
zero kama mwaka huu tumepeta division one 6, 2024 tuhakikishe tunapata division
One zote” Mohammed Abrahman Mwinyi
Kwa upande wake katibu mwenezi wa
chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mkaoni Talib Bailal Shamte, amesema kutolewa
kwa zawadi hizo ni kuwaongezea ari wananfunzi hao ili kuhakikisha wanafanya
vizuri katika masomo pamoja na mitihani yao ya kidato cha sita.
“Tumeamua kuwapatia hizi zawadi ili
ziwe ni chachu ya nyinyi kuwa na shauku na ari ya kuendelea kusoma kwa bidii ili
muendelee kufanya vizuri katika masomo yenu na mitihani yenu ya kidato cha sita
kwahivyo nawaombeni musome kwa bidii sana na sisi tuko nyuma yenu” Talib Bilal
Nae katibu wa CCM jimbo la Chambani Amour
Kheri Vuai, amewataka wanafunzi hao kutokujiingiza katika suala la mapenzi ili kuimarisha
msingi wa maisha yao ya baadae.
“Nawasihi sana kutokujiingiza katika suala la mapenzi kwasababu mukishajiingiza tu kwenye mapenzi safari ya masomo imeishia hapo kwahivyo sasa hivi kazi yenu iwe ni kusoma tu na sio vyenginevyo” Amour Kheri Vuai
Shaibu Ali Juma ni mwenyekiti wa CCM jimbo la Chambani , amesema kutolewa kwa zawadi hizo ni muendelezo wa kutekeleza kwa ahadi mbali mbali zilizotolewa na viongozi wa jimbo katika kuunga mkono juhudi za maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo.
Diwani wa wadi ya Ngwachani Mohammed
Said Ali, amewaomba wanafunzi hao kuchagua masomo ambayo yataendana na fani ambazo
wanajiandaa kusomea ili kwenda sambamba na fani hizo.
“Suala la kutambua ni nataka kuwa
nani katika maisha yako ya baadae kisha ukatambua masomo ya kusoma ni muhimu
sana kwani utakaposhindwa kutambu
unahitaji kuwa nani hapo baadae utashindwa kujua ni masomo gani muhimu ya
kusoma” Diwani Mohammed Said
Nao wanafunzi hao wameushukuru uongozi
wa jimbo hilo kwakuwapatia zawadi hizo na kuahidi kusoma kwa bidii ili kufanya
vizuri katika mitahani yao ya kidato cha sita.
“Kwakweli tumefarijika sana kwakuaptiwa zawadi hizi na inatia moyo kuwa viongozi wa jimbo letu wako pamoja nasi kwahivyo tunaahidi kusoma kwa bidii ili kufanya vizuri katika mitahani yetu ya kidato cha sita” Aziza Amour Salehe kutoka Skuli ya Sekondari Ukutini