Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima ametoa siku tatu kwa Mkandasi anayejenga Jengo jipya la Ofisi ya Wizara ahakikishe anaweka Kalenda ya ujenzi ndani ya siku tatu kuanzia leo ili iwe rahisi kwa ufuatiliaji na tathmini ya kujua kama kuna kasi nzuri ya maendeleo kwenye ujenzi huo unaotazamiwa kuchukua miezi 24 Juni, 2024.
Dkt. Gwajima ametoa maagizo hayo mapema leo Julai 13, 2022 Mara baada yakufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi.
"Nimefika hapa nikiwa na Naibu Waziri wangu Mwanaid Ally Khamis (Mb) kwa lengo la kukagua hali ya ujenzi ambapo tumemkuta Mkandarasi anaendelea lakini kubwa baada ya ukaguzi nimeagiza Mkandarasi kuandaa Kalenda ya Ujenzi ambayo ndio itakuwa 'Road Map' kujua kama kazi inakwenda kwa Kasi stahiki au la" amesema Dkt. Gwajima.
Dkt. Gwajima amemshukuru pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa maono yake ya kuanzisha Wizara lakini kikubwa kuwapatia eneo la kuweza kujenga Ofisi ya Wizara.
Waziri Gwajima amesema Jengo hilo la Ghorofa Nane, litagharimu Bil. 29.9 hadi kukamilika kwake
Kwa upande wake Naibu Waziri Mwanaidi Ally Khamis ambaye ndiye Msimamizi Mkuu wa Miradi ya Wizara amesema atasimama imara katika kusimamia na endapo atabaini kuwepo kwa mapungufu hatosita kumwambia Mkandarasi bomoa na kujenga upya.
Akitoa ahadi mbele ya Viongozi hao, Mkandarasi Michael Mussa, amesema amepokea maelekezo yote ya Wizara na kwa kutumia uzoefu wake wa miaka saba atahakikisha anakamilisha kazi hiyo kwa wakati nabkwa viwango vilivyokubalika.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum ni Wizara Mpya kabisa ambayo ilikuwa Januari 08, 2022.
TAZAMA VIDEO HII YA WAZIRI DOROTH GWAJIMA