Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia watu wawili ambao ni Omary Lucas, Miaka 48, Mkazi wa Buhongwa ambaye ni mume wa marehemu na Amos Lucas , Miaka 29, Mlinzi, Mkazi wa Isabenda kwa tuhuma za kosa la mauaji ya Elizabeth Lusana, Miaka 61, Mkazi wa mtaa wa Kagera, kata ya Lwanhima, Wilaya ya Nayamagana aliyeuawa Julai 11 mwaka huu kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali maeneo mbalimbali ya mwili wake.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ramadhan Ng'anzi amesema uchunguzi wa awali umebaini wanandoa hao walikuwa na ugomvi uliotokana wivu wa kimapenzi ambapo mwanaume alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa na mahusiano yasiofaa nje ya ndoa ulio pelekea mauaji hayo.
Kamanda Ng'anzi amesem mtuhumiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo alitoroka na kwenda kujificha mkoani Tabora kwa Amos Lucas, lakini ufatiliaji wa Polisi uliweza kubaini mahali alipo na kuwakamata yeye pamoja na mtu aliyemficha.
Katika tukio la pili Jeshi la Polisi jijini hapa limemkamata Said Furaha Miaka 31, Msukuma, Mkazi wa Nundu, Mfanya biashara, kwa kosa la kupatikana na jezi bandia dazani 145 zenye nembo ya club ya simba zinazo milikiwa na kampuni ya VUNJA BEI na jezi dazani 151 zenye nembo ya Club ya Yanga zinazo milikiwa na kampuni ya GSM, kitendo ambacho nikinyume na sheria.
Awali Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka kwa afisa masoko wa kampuni ya GSM na VUNJA BEI kuwa hapa Jijini Mwanza kuna mfanya biashara anae sambaza na kuuza jezi bandia.
Hata hivyo, baada ya taarifa hizo ufatiliaji wa kina na haraka ulifanyika na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na jumla ya dazani 296 bandia za club ya Simba na Yanga dukani kwake eneo la Pamba.