MTOTO WA MIAKA SITA ABAKWA AKIENDA DUKANI

0
Picha kutoka Maktaba

Mtoto mwenye umri wa miaka sita ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kimaadili amebakwa katika kijiji cha ibindi halmashauri ya manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi huku wakazi wa eneo hilo  wakieleza kuwa na hofu sana kutokana na matukio ya ubakaji kujitokeza mara kwa mara.

Akizungumza  mama mzazi wa mtoto huyo akiwa katika hospital teule ya rufaa Mkoa wa Katavi ambako amempeleka mtoto huyo kupatiwa matibabu baada ya kufanyiwa vitendo vya kikatili .


Vitendo hivi vya ukatili katika kijiji hicho cha Ibindi imeelezwa kuwa vimeleta hofu ndani ya jamii ikiwa ni baada ya mtoto mwenye umri wa miaka sita kufanyiwa udhalilishwaji ambapo baadhi ya wanawake wamesikitishwa na kuiomba serikali iwasaidiwe kutokomeza matukio hayo.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ambaye pia ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya Bi Jamila Yusuph amewahakikishia wanawake wa kijiji hicho serikali kulifatilia jambo hilo na kuwaasa kuacha tabia ya kuvuruga kesi pindi wanapotakiwa kutoa ushahidi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top