MUHIMBILI WAMLILIA NEEMA PACHA ALIYEFARIKI AKIPATIWA MATIBABU.

0

Pacha waliotenganishwa

Mmoja wa pacha aitwaye Neema waliotenganishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili amefariki dunia Julai 10, 2022. Aidha mwenzake aitwaye Rehema anaendelea vizuri.

Taarifa iliyotolewa na Hospitali hiyo Julai 12, 2022 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Aminiel Aligaesha, imeeleza kuwa hali ya Neema ilibadilika ghafla akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

"Tuendelee kumuombea Rehema ambaye bado yupo ICU ili Mwenyezi Mungu amjalie afya njema. Bwana alitoa na Bwana ametoa, jina lake lihimidiwe sana," amesema Aligaesha

Mapacha hao Neema na Rehema, walifanyiwa upasuaji Julai Mosi mwaka huu, ambapo kwa mujibu wa hospitali hiyo upasuaji huo ulifanyika na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top