MUME ADAIWA KUMUUA MKE NAKUMTUPA NJE WAKISUBIRI MAHARI YA BINTI YAO

0

Mzee aliyefahamika kwa jina la Ezekiel Jacob mkaazi wa kata ya Leguruki wilayani Arumeru mkoani Arusha anatuhumiwa kumuua mkewe Walialanga Gidion kwa kumnyonga na kumvunja shingo siku moja kabla ya sherehe ya binti yao ya kuletewa mahari nyumbani kwao.

Picha haihusiani na tukio halisi (Picha kutoka Maktaba)

Imeelezwa kuwa Mzee Jacob anatuhumiwa kufanya mauaji hayo wakati binti yake aitwaye Anjelina Ezekiel akiwa njiani kurejea nyumbani kwa ajili ya kushuhudia tukio la kutolewa na mahari.

Akizungumza Silasi Mbise Mshili mkuu wa ukoo wa Mbise Meru amesema mzee Ezekiel anashikiliwa na jeshi la polisi na aliwahi kutoa kauli za vitisho za kumuua mkewe siku moja.

'Kulikuwa na ahadi kwamba nitakuua,sababu hazijulikanai,alikuwa amemvunja mkono na si mara moja imekuwa sababu ya kudhihirisha amemuua kweli' amesema mbise.

Familia ya mtuhumiwa Ezekiel Jacob imekiri ndugu yao kuhusishwa na mauji hayo na kutoa ndama kwa ajili ya kuomba msamaha na baadae watatakiwa kulipa ng'ombe 49 kutekeleza mila ya jamii hiyo inavyotaka.

'Atalipa fidia kama jadi na mila inavyotuongoza,alipe fidia kwenye ukoo wa kitomali, atalipa ng'ombe 49 pamoja na garama zilizotumika,na watakao lipa ni ukoo wake sio yeye na tumekubaliana wao waende kujadiliana na Polisi ili serikali ikikubali aachiwe ili awajibishwe kwa asili ya tangu jadi' amesema mbise.

Akizungumza Mzee Israel Kitomali amesema usiku wa ijumaa walipokea taarifa ya msiba wa ndugu yao,na kwamba wao kama familia wanaendelea na mazungumzo juu ya hatima ya tukio hilo.

'Tulipofika kule tukakuta tayari dada yetu ameshafariki lakini hataukupata jambo lingine zaidi ya kifo ila baada ya muda walikuja polisi wakamchukua mumewe pamoja na kupakia mwili wa marehemu na kuondoka nao'alisema kaka wa marehemu Kitomali.

Kwa sasa Mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi kufuatia kifo cha mama huyo.

TAZAMA  TUKIO ZIMA HAPA LA MAUJI YA MWANAMKE KUTOKA MILLARDAYOTags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top