MUME ADAKWA KWA TUHUMA ZA MAUJI YA MKEWE WAKIWA UKWENI

0

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata Selemani Malima maarufu Jiwe Mkazi wa Keko Mwanga kwa tuhuma za mauaji ya Mke wake Husna Majaliwa (21), aliyekuwa mkazi wa Goba kwa Awadhi kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali tumboni.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam amesema “Tukio hilo lilitokea June 12, 2022 huko maeneo ya Goba, Kinondoni na mara baada ya tukio hilo alitoweka”

“Uchunguzi wa awali unaonesha kulikuwa na mgogoro wakifamilia baina ya wawili hao na mtuhumiwa alifika nyumbani kwa wazazi wa marehemu kumsalimia Mzazi mwezake pamoja na Mtoto wakati wakiwa katika maongezi ndipo mtuhumiwa alimshambulia kwa kisu Mke wake na kumsabishia kifo”

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam lilifanya ufuatiliaji wa kina na July 18, 02022 lilifanikiwa kumkamata Mtuhumiwa huyo huko Mbande Jijini Dodoma alipokuwa amejificha na baada ya mahojiano ya kina, Mtuhumiwa ameonesha kisu alichotumia kumuua mke wake, uchunguzi unakamilishwa na Mtuhumiwa anatafikishwa Mahakamani haraka izwekanavyo”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top