MUME AJIUA BAADA YA MKEWE KUGOMA KURUDIANA NAE

0

Mwanaume mmoja alijiua ka kujipiga risasi eneo la Muthangari jijini Nairobi baada ya mke wake waliyekosana kukataa kumrudia.


Iyaz Mukhi mwenye umri wa miaka 63 alienda kwa nyumba ya mwanamke huyo ambaye walikosana na kutengana Septemba mwaka jana kwa sababu za kinyumbani. 

Lengo kuu la mfanyabiashara huyo lilikuwa kumshawishi mkewe amrudie, na alianza kwa kuomba msamaha na kuendelea kumrai mama wa watoto wake wawili kumrudia lakini rai zake ziligonga mwamba.

Baada ya ombi lake kukataliwa, Mukhi alichomoa bastola yake aina ya Glock na kujipiga risasi katika nyumba ya mwanamke huyo huku waliokuwepo wakikimbia kwa kuhofia usalama wao.

 Bastola ya Glock na vazi la risasi moja iliyotumika vilipatikana eneo la tukio,” taarifa ya polisi inasema.

 Kwa mujibu wa polisi, mwendazake alikuwa na leseni ya kumiliki bunduki na bastola aliyokuwa nayo ilikuwa na risasi 12.

Visa vya watu kujitoa uhai vinazidi kuongezeka huku polisi wakirekodi angalau visa viwili kila siku.

Mwaka 2019, watu 499 walijitoa uhai huku watu 575 wakijiua mwaka 2020. Japokuwa polisi wangali kutoa takwimu za mwaka huu, inaripotiwa kuwa watu 313 wamejitoa uhai kati ya Januari na Julai 2022.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top