MWALIMU MBARONI KWA KULAWITI WANAFUNZI WATATU BWENINI

0

 Mwalimu wa kiume anazuiliwa katika Kaunti ya Bomet baada ya kudaiwa kuwalawiti wanafunzi watatu wenye umri wa kati ya miaka 11 na 13. 

Mshukiwa huyo alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Mogogosiek huko Konoin na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kutokana na vitendo hivyo vya kinyama katika Chuo cha Mosoriot. 

Mkuu wa polisi wa Konoin Tom Achiya alisema mshukiwa, Bernard Kirui, alikamatwa baada ya mmoja wa waathiriwa kulalamika kwa maumivu makali na kukimbizwa katika Hospitali ya Misheni ya Litein; ambapo ilithibitishwa kuwa alikuwa amelawitiwa.

 "Kukamatwa kwake kunafuatia malalamiko kutoka kwa wafanyakazi wa shule hiyo. 

Tulifanya uchunguzi jambo ambalo lilipelekea mshukiwa kukamatwa," Achiya alisema.

 Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mkuu huyo wa shule alilala kwenye bweni la wavulana licha ya kutengewa chumba chake na shule. 

"Tunafikiria kufunga shule ili kupisha uchunguzi huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa wazazi na jamii," Chifu wa Koiwa Emmy Ngetich aliambia Citizen Digital.

 Mshukiwa anatarajiwa katika Mahakama ya Sheria ya Sotik mara tu polisi watakapokamilisha uchunguzi wao.

TAZAMA VIDEO HII KUJIFUNZA KUTENGENEZA PESA MTANDAONI.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top