Mwili wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta (JKUAT) umepatikana ukining’inia katika nyumba yake mjini Juja, Kaunti ya Kiambu katika kile kinachokisiwa kuwa kisa cha kujitoa uhai kwa kushindwa kufaulu katika masomo yake.
Maafisa walisema kuwa sehemu ya kwanza ya uchunguzi inaonyesha kuwa Irene Monica Mwangi mwenye umri wa miaka 26 na mwanafunzi wa Kompyuta ya Biashara alijinyonga baada ya kukosa kufaulu mitihani yake.
Mwili wake ulipatikana kwenye mlango wa bafu la nyumba yake ya kukodi mjini Juja ambapo imeonekana alitumia kitambaa kujinyonga.
Haya yalitokea huku wanafunzi wengine ambao walikuwa wamemaliza masomo yao wakifuzu mnamo Juni 28 mwaka huu huku monica akiwambia wenzake kuumizwa kwa kushsindwa kuhitimu pamoja nao.
Polisi wanasema kuwa waliitwa eneo la tukio siku ambayo hafla ya kufuzu kwa mahafala ilikuwa ikiendelea na kuugundua mwili huo,Barua ya kujitoa uhai ilipatikana katika chumba hicho na vilivyokuwa ndani kufahamishwa familia.