Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linamshikilia Jonas Ziganyige (71) Mstaafu wa Jeshi la Wananchi, Mkazi wa Mbezi juu kwa tuhuma za kumpiga risasi na kumuua Patient Romwadi (48) Mfanyabiashara, Mkazi wa Wazo Mivumoni, Kinondoni.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM Muliro Jumanne amesema “Taarifa za awali, zinaonesha kuwa tarehe 09.07.2022 majira ya saa 4 asubuhi Recy Renso (52) Mkazi wa Posta alifika eneo hilo na Mtu huyo ambaye ni marehemu kwa sasa kwa lengo la kuangalia mipaka ya kiwanja chake, Mtuhumiwa alitoka ndani huku akionesha kukasirishwa na hatua ya Waty hao, akachukua bunduki na kumpiga risasi Patient Romward ambaye baadae alifariki”
“Baada ya tukio hilo Mtuhumiwa alikimbia lakini upelelezi ulifanywa haraka na tarehe 10.07.2022 alikamatwa eneo la Kibaha Maili Moja akiwa amejificha”
“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam pia limeipata silaha aliyotumia mtuhumiwa ambayo ni aina ya Mark IV ikiwa na risasi 4, Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo kujibu mashtaka yanayomkabili”