Kufuatia takwimu za sensa ya 2012 kubainisha kwamba mkoa wa Njombe wenye halmashauri 6 unawakazi 702,097 tu! Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoani humo Jasel Mwamwala ametoa wito kwa wanaume wa mkoa huo kuoa mke zaidi ya mmoja na kupata watoto wengi iwezekanavyo ili kuujaza mkoa huo ambao unatajwa kuwa na idadi ndogo ya watu licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa vyakula na rasilimali.
![]() |
Picha kutoka Maktaba |
Mwamala ametoa kauli hiyo wakati wa kuhitimisha mafunzo ya sensa ya watu na makazi kwa wakufunzi 144 ambao watakabidhiwa jukumu la kutoa elimu kama hiyo kwa makarani wapatao 3665 ambapo amesema kunasababu ya kuongeza kasi ya kuzaliana ili kuongeza idadi ya watu ili sensa itakapofanyika wakati mwingine serikali itumie takwimu hizo kutenga fungu kubwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Katika kuhakikisha wazo lake linapokelewa na kutiliwa mkazi Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Njombe anasema ameshafanya jitihada za kukutana na viongozi wa dini na makundi mengine ili kuhamasisha wafuasi wao kuzaliana kwa kasi na kisha kusema kwamba kabla ya kutundika garuga katika uga wa kisiasa angetamani kuona iadadi ya watu inaongezeka nyumbani kwake Makete ambako hadi sasa kuna wakazi chini ya lakimbili.
Awali akiweka bayana miiko na faida ya zoezi hilo kitaifa na kimataifa mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba anasema ni kosa kubwa kwa karani na waratibu kutumia lugha chafu wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo ili kupata ushirikiano kwa wananchi na takwimu sahihi ambazo ndiyo zitakuwa dira ya maendeleo yetu katika miaka 10 iyayo.
Miaka ya Nyuma jamii nyingi zilikuwa na mtazamo tofauti juu ya sensa jambo ambalo limeisukuma serikali kuwahisisha kwa karibu viongozi wa dini na machief kukamasisha wananchi kujitokeza kuhesabishwa kama ambavyo Charles Mkongwa chief wa mkoa wa Njombe anavyobainisha na wahitimu wa mafunzo hayo wanabainisha wanachokwenda kufanya
Takwimu zilizotolewa na serikali kwa mara mwisho baada ya kufanyika sensa ya 2012 mkoa wa Njombe ulikuwa na wakazi 702079 ,Swali ni watu wangapi wameongezeka kuanzia 2012 hadi mwaka huu 2022.
TAZAMA VIDEO HII MWENYEKITI AKITOA KAULI YA KUZUNGUMZA NA WACHUNGAJI NA MASHEKHE.