MWIZI MBARONI KWA MAUAJI YA BINTI WA KAZI AKIFANYA WIZI

0

 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata na linamshikilia Selemani Haruna maarufu Kwata (24), Mkazi wa Kimara Temboni mtaa wa Amani, kwa tuhuma za kumuua Editha Charles (22) Mkerewe, Binti wa kazi za ndani na kuuficha mwili huo katika stoo ya vifaa vya ujenzi katika nyumba ya Agatha Stanslaus.Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Jumanne Muliro amesema “Uchunguzi wa awali umeonesha Mtuhumiwa tarehe 06/07/2022 asubuhi alifika kwenye nyumba aliyokuwa anayoishi Binti huyo wa kazi akijifanya fundi wa umeme na kwamba alitakiwa kuweka Balbu, alipoingia alimshambulia kwa kitu chenye ncha kali Binti huyo na kumuua halafu akavunja chumba cha mwenye nyumba na kuiba Tsh 1,800,000 na kutoweka”

“Polisi kwa Kutumia Watalaamu wake wa uchunguzi wa kisayansi na vyanzo vingine vya kiuchunguzi walibaini Mtuhumiwa huyo kuwa aliingia kwenye nyumba hiyo na kukaa kwa masaa kadhaa na kutoka, baada ya kumkamata na kumhoji kwa kina alikiri kumuua Binti huyo, kuvunja mlango wa chumba na kuiba pesa Tsh 1,800,000 na mwili wa marehemu aliuficha kwenye stoo ya nyumba hiyo huku akiwa ameufunika na vifaa mbalimbali vya ujenzi ili usionekane”

“Alionesha pesa alizoziiba eneo hilo na pesa nyingine alidai mara baada ya tukio siku iliyofuata alinunua simu mpya, viatu vya mpira pea 2, na begi la mgongoni lenye nguo mbalimbali mpya ambavyo navyo vimepatikana, kitendo alichofanya Mtuhumiwa ni cha ukatili ulipita kiasi, uchunguzi wa shauri hili unakamilishwa na atafikishwa katika mifumo ya kisheria ikiwemo Mahakamani haraka” amesema Kamanda.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top