Mahakama ya Mji wa Minneaolis, Minnesota nchini Marekani imemuhukumu kitumikia kifungu cha 21 na nusu jela ofisa wa polisi, Derek Chauvin baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Mmarekani mweusi, George Floyd Mei mwaka 2019 na kusababisha maandamano makubwa yaliyotikisa dunia.
Chauvin anakwenda baada ya Mahakama na Minnesota kujiridhisha pasipo na shaka kuwa Derek alitenda makosa ya kutumia vibaya nafasi aliyoaminiwa na mamlaka yake kisha kufanya ukatili dhidi ya Floyd, kitenda kosa hadharani huku watoto wakishuhudia na kutenda kosa kwa kushirikiana na watu wengine watatu kinyume na sheria za Minnesota.
“Ninatoa salamu zangu za pole kwa
familia ya Floyd” haya yalikuwa maneno ya ya mwisho ya Chauvin kabla ya hukumu
kusomwa.
Kwa mujibu wa sheria za Minnesota,
Chauvin atatakiwa kutumikia robo tatu za au miaka 15 kifungo jela.
Kwanini hii ni hukumu ya Kihistoria?
Kwa mujibu wa mwongozo wa utoaji wa
adhabu mjini Minnesota mtu anapaswa kufungwa jela kwa mud usiozidi miaka 10
hadi 15 ambacho ni kiwango cha juu cha adhabu dhidi ya makosa ya jinai, lakini
kwa Chauvin mwongozo huo umewekwa kando na atatumikia adhabu kwa kipindi miaka
21 na miezi sita.
Jaji aliyesikiliza kesi hiyo, Peter
Cahill alisema adhabu hiyo haijafuata mihemko wala mawazo ya mtu.
“Nimezingatia zaidi maumivu ambayo
familia ya Floyd imeyapata na inayo hadi leo” ameandika jaji Cahill katika
hukumu hiyo iliyochapishwa kwenye kurasa 22, ikitajwa kuwa hukumu kali mno kwa
Chauvin.
Makosa mengine ya Chauvin ni kutumia
vibaya nafasi yake kwa pamoja na mamlaka aliyopewa.
Katika hukumu hiyo, Jaji Cahill
alisema Chauvin bila heshima alimdhulumu Floyd “utu” wake ambao ni haki ya kila
binadamu.
Picha ya video iliyomuonyesha Chauvin
akimkandamiza goti la shingo Floyd bila kumpa nafasi hata ya kupumua kwa muda
mrefu ni dhahiri alimsababishia maumivu yasiyomithilika.
“Yalikuwa mauaji ya maumivu na mateso
ya kiwango cha juu sana” inasomeka sehemu ya hukumu ya Jaji Cahill.
Kesi hii pia inabaki kuwa ya
kihistoria katika mwenendo wa usikilizwaji wake baada ya kumkuta Chauvin na
hatia
Jopo la waendesha mashtaka wa
Serikali lilipendekeza apewe adhabu ya miaka 30 jela hatua ambayo jopo hilo lilisema
inaweza kuifuta zaidi machozi ya familia ya Floyd na jamii ya watu weusi.
Hata hivyo, Chauvin aliiomba Mahakama
impunguzie adhabu kwa kutazama historia yake kuwa hana historia yoyote ya
kutenda makosa nchini humo.
Ilivyokuwa
Chauvin alitenda kosa hilo akiwa na
wenzake watatu eneo la tukio, Tou Thao Thomas Lane na Alex Kueng.
Akiwa na wenzake Chauvin alimuua
Floyd kwa kumbana shingo kwa nguvu akitumia goti kwa muda wa dakika 9 na
sekunde 29 bila ya kumpa punzi na alisikika akilalama kwa mbali kuwa hawezi kupumua
alipokamatwa na askari huyo kwa madai ya kufanya malipo katika duka moja kwa
kutumia noti bandia.
Vitendo vya polisi kuua raia Marekani vilikuwa vikiongezeka mara kwa mara, ndani ya miezi mitano ya mwaka 2021, watu 371 walifyatuliwa risasi na polisi kati yao 71 wakiwa watu weusi.
Mwaka 2020 hali hii ilitajwa kuwa
mbaya zaidi ambapo watu 1,021 walipigwa risasi na polisi.
Katika matukio hayo ndani ya miaka
miwili, idadi ya Wamarekani weusi inaongoza kwa kushambuliwa kwa risasi na
polisi ikilinganishwa na makundi mengine yanayopatikana nchini humo.