VIDEO; IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA WANAFUNZI YAFIKIA 13

0

 Watu 13 wakiwemo wanafunzi nane (8) wa Shule ya Msingi ya King David iliyopo mkoani Mtwara wamefariki dunia katika ajali ya gari la shule hiyo iloyotokea katika eneo la Mjimwema, Manispaa ya Mtwara Mikindani Julai 26, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali, Marco Gaguti amethibitisha kuongezeka kwa vifo vya Wanafunzi wawili wa Shule ya King David ambao walikuwa miongoni mwa majeruhi Watano waliokuwa katika hali mbaya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Ligula.

Vifo vyao vinafanya idadi ya vifo kufikia Watu 13 huku wawili kati yao wakiwa ni Dereva na Mwangalizi mmoja wa Wanafunzi ambapo miili ya Wanafunzi hao imeagwa leo katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameeleza kusikitishwa taarifa za Watu 10 wakiwemo wanafunzi nane (8) waliofariki dunia katika ajali ya Basi dogo la wanafunzi wa Shule ya Msingi King David iliyoko mkoani Mtwara iliyotokea leo Asubuhi maeneo ya Mjimwema, Mikindani.

"Nimesikitishwa na vifo vya wanafunzi 8 wa Shule ya Msingi King David na watu wazima wawili vilivyotokea leo eneo la Mjimwema, Mikindani, mkoani Mtwara."

"Natoa pole kwa wote waliopoteza jamaa zao. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema na awajalie majeruhi wapone haraka." -  Rais

TAZAMA VIDEO YA AJALI HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top