Mahakama ya Wilaya ya Makete mkoani Njombe imemuhukumu Bahati Langson Sanga mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa kijiji cha Ihanga wilayani Makete Mkoani Njombe kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kulawiti.
Aprili 17, 2022 majira ya usiku mshtakiwa huyo Bahati Sanga alimlawiti kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 20 (jina limehifadhiwa) wakati akitoka kusherehekea sikukuu ya Pasaka kosa ambalo ni kinyume na sheria kifungu cha 154 (1)(a) cha sheria ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo 2019
Soma hii :App nzuri kuediti Picha kwa SIMU 2022 hii hapa
Upande wa mashahidi wa jamhuri akiwemo mlalamikaji mwenyewe ameiambia mahakama kuwa siku ya tukio majira ya usiku wakati akirudi nyumbani alikutana na mshtakiwa huyo ndipo alipompeleka kwenye nyumba yake na kumfanyia kitendo hicho huku akitishia kumuua pindi atakapomwambia mtu.
Kwa upande wa mashtaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa polisi Inspekta wa Polisi Benstard Mwoshe umeiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho na kwa wengine wanaofikiria kutenda kosa kama hilo.