SEARCH FOR COMMON GROUND KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI ZOEZI LA SENSA

Hassan Msellem
0

Wananchi Kisiwani Pemba wametakiwa kushiriki ipaswavyo katika Zoezi la sensa ya watu na Makaazi ili kutimiza azma ya Serikali katika kuwaletea wananchi Maendeleo.

                                                                                                    Akizungumza katika mkutano wa siku moja na wadau wa Amani Zanzibar Afisa Mdhamini kutoka afisi ya Rais tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Pemba Mhe. Thabit Othman Abdallah ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo uliofanyika huko katika ukumbi wa Hoteli ya Green Foliage Mgogoni Chake Chake, amesema zoezi la Sensa ni sehemu ya kutunza amani ya nchi kwani Serikali hupata nafasi ya kuratibu mipango ya maendeleo watu wake

Ameongeza kuwa ni vyema kuzihamasisha familia zetu kupunguza mizunguko na safari zisizo na ulazima katika usiku wa kuamkia tarehe 23 ili kuwapunguzia usumbufu makarani na watendaji wengine wa sensa na kufanikisha kwa usahihi zoezi hilo.

Kwa upande wake afisa habari wa Shirika la Seach for Common Ground Khelef Nassor Rashid amesema jamii lazima iafikiane na suala la amani ili kuiwezesha serikali kufanikisha sera yake ya uchumi wa buluu kwa maendeleo ya wanannchi.


Kwani amesema bila ya Amani sera hiyo haitotekelezeka, hivyo ni wajibu wa kila mwanajamii kudumisha Amani iliyopo ili taifa liweze kufanikisha malengo yake.

  Amesema bila ya Amani hakuna maendeleo na kutolea mfano wa yanayotokea nchini Ukrein na Russia kwa sasa kwa kusema kuwa vita ni jambo baya lakulijengea mazingatio kwani licha ya wao wenyewe kupata mkwamo wa kiuchumi lakini dunia pia imeingia katika mgogoro wa kimaslahi kwa kupanda bei za bidhaa ulimwenguni kote.

 Mkutano huo wa siku moja wa kongamano la Amani kisiwani Pemba ulifanyika chini ya mradi wa dumisha Amani Zanzibar unaoendeshwa na Shirika la Search for Common Ground wakishirikiana na taasisi ya Fondotion for Civil Society chini ya ufadhili wa European Union(EU).                                                                     

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top