SERIKALI KUTOA UFAFANUZI NYONGEZA YA MISHAHARA KESHO TUCTA

0
 Serikali ya Tanzania Jumatatu Julai 26, 2022 itakutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) ili kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara Julai mwaka huu.
Taarifa hiyo imetolewa Jumapili, Julai 24, 2022 na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa katika ukarasa wake wa mtandao wa Twitter.
“Ndugu wafanyakazi, Jummane tarehe 26 Julai 2022 Serikali itakutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) ili kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara katika mishahara ya Julai 2022,”amesema.

Itakumbukwa  kuwa Rais Samia Suluhu Hassan aliridhia mapendekezo ya kuongeza mishahara ikiwemo kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa asilimia 23.3, ambapo Sh1.59 trilioni itatumika kwa ongezeko hilo.
Katika taarifa iliyotolewa Mei 14 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus inasema mapendekezo hayo ni mwendelezo wa kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alichokifanya hivi karibuni mkoani Dodoma na kupokea taarifa kutoka kwa wataalamu kuhusu ongezeko la mishahara.
Taarifa hiyo ilisema Serikali imepanga kutumia kiasi cha Sh9.7 trilioni katika mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishara ya watumishi wote katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na Wakala za Serikali.
“Bajeti ya mishahara ya mwaka 2022/23 inaongezeko la Sh1.59 trilioni sawa na asilimia 19.51 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021/22,” imesema taarifa hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top