SERIKALI YATOA KAULI ALIYEKUTWA AKITOKWA DAMU WILAYANI MAKETE...

0

Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Tandala wilayani Makete mkoani Njombe wamekumbwa na hali ya taharuki baada ya kuona Bw.Deo Sanga ambaye ni mkazi wa Tandala anatokwa na damu mfululizo puani huku wakimhusisha na ugonjwa wa kutokwa damu uliotokea mkoani Lindi.

Tukio hilo limetokea Julai 18,2022  majira ya mchana kando ya barabara ya kuelekea chuo cha Ualimu Tandala ambapo baadhi ya watu walikuwa wakiendelea na shughuli zao ndipo waliposhuhudia mtu huyo akitokwa na damu mfululizo puani

Baadhi ya wananchi waliokuwepo katika eneo la tukio wamesema kuwa alianza kutokwa na damu mfululizo hali iliyowafanya baadhi yao waanze kuogopa ambapo kwa hatua za awali walianza kumpa huduma ya kwanza kwa kumlaza chali na kumziba puani kwa pamba

Hata hivyo wamesema kuwa kutokana na ugonjwa ulioripotiwa hivi karibuni mkoani Lindi waliona ni vizuri kuwasiliana na vyombo vya habari ili viweze kuwasiliana na mamlaka husika kwa ajili ya kumfanyia uchunguzi mtu huyo.

Baada ya mwandishi wetu kufika katika eneo hilo imezungumza na mtu huyo ambapo amesema amekuwa na historia ya kutokwa na damu lakini kilichomshangaza ni baada ya kuona damu inatoka kwa wingi puani tofauti na vile ambavyo imekuwa ikitoka kwa siku za kawaida.

Akiwa Katika eneo la tukio mwandishi wa habari wa  amempigia simu Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Makete Dkt.Ligobert Kalisa ambapo amemhoji baadhi ya maswali mtu huyo na kuagiza apelekwe hospitali ya Consolata Ikonda kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam.

Baada ya kufanyiwa vipimo mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Makete amezungumza  na kueleza kuwa baada ya kufanyiwa vipimo imeonesha kuwa mtu huyo alikuwa na tatizo la muda mrefu la kutokwa na damu hasa presha inapopanda,hivyo hana ugonjwa wa kutokwa damu unadaiwa kutokea mkoani Lindi.

TAZAMA VIDEO YA TUKIO LA MWANANCHI HUYO ALIYEHOFIWA KUWA NA UGONJWA WA MGUNDA.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top