TAMWA YAVIOMBA VYOMBO VYA HABARI KUANZISHA MADAWATI YA KIJINSIA.

Hassan Msellem
0

Chama cha Waandishi wahabari Waanawake Tanzania (TAMWA-ZNZ) kinaviomba vyombo  vya habari  Nchini kuweka madawati ya kijinsia ili kushughulikia kwa ukaribu masuala hayo na hivyo kuimarisha haki za zawanawake na watoto. 


TAMWA-ZNZ hivi karibuni ilitembelea vyombo vya habari 14 (10  kutoka Unguja na 4 kutoka Pemba) vikiwemo vyombo vya Habari vya umma, binafsi na radio za kijamii.MKURUGENZI WA TAMWA-ZANZIBAR DKT. MZURI ISSA

Afisa wa ufuatiliaji na Tathmini wa TAMWA- ZNZ Bwana Mohammed Khatibu alisema katika ziara hiyo iliyoanza tarehe 24 Mei hadi 21 Juni , TAMWA,ZNZ ilikuta vyombo vya habari vitatu ambavyo vimeweka madawati ya kijinsia na vilivyobaki bado havikuanza utaratibu huo.


Alisema pia baadhi ya vyombo vya habari asilimia 33% vilikuwa na sera ya jinsia ambayo ni muhimu kwa usawa wa kijinsia lakini nyingi zao zilikosa mipango kazi wa utekelezaji wa sera hiyo.Hivyo, alisema TAMWA- ZNZ itakaa pamoja na vyombo hivyo kuandaa mpango kazi wa utekelezaji pamoja na kuweka na mfumo maalum wa kuripoti matokeao yake. 


Vyombo vya habari vikiwa na mifumo ya kijinsia vitasaidia sana kutoa habari ambazo zinauwiano sawa wa kijinsia, kutafuta mambo ambayo yanaawaathiri wanawake pamoja na kutoa sauti za wanawake na watoto wa kike hivyo kuongeza kujiamini kwao; jambo ambalo ni muhimu katika safari yao ya uongozi. 


Uchambuzi wa kihabari uliofanywa na TAMWA- ZNZ mwaka jana (2021) ulioonyesha  kuwa ni asilimia 25 tu ya habari ndiyo imebeba sauti za wanasiasa wanawake na  hivyo kuna haja ya kuleta uwiano hasa kwa vile wanawake ni zaidi ya asilimia 50 ya wakaazi wa Zanzibar kwa mujibu wa takwimu za sensa ya mwaka 2012 na makadirio yake. 


Tanzania pamoja na Zanzibar zimeridhia Itifaki mbali mbali za kimataifa pamoja na za kikanda ili kuhalikisha  inatekeleza  azimio la kufikia usawa wa kijinsia ikiwemo uwakilishi wao katika vyombo vya maamuzi na sauti zao katika vyombo vya habari. 


Hata hivyo, TAMWA- ZNZ inashukuru kwa mapokezi iliyopewa na vyombo vya habari mbali mbali, ambapo pia vimekubaliana kuweka madawati na sera za kijinsia pamoja na kuweka mikakati ya utekelezaji wake.


Akizungumza wakati wa mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar, Bwana Salum Ramadhan Abdalla ameeleza utayari wa Shirika lake katika kuimarisha habari za kijinsia ikiwemo kuweka mfumo wa kumbukumbu na ufuatiliaji wa masuala ya kijinsia. 


“Tupo katika mchakato wa kutengeneza sera ya jinsia, hivyo haya yote tutayazingatia ili tuweze kuripoti habari za wanawake kama wasemaji, lakini pia kama walengwa wa taarifa zetu”, alisema. 


Chama cha waandishi wahabari waanawake Tanzania (TAMWA-ZNZ) kinaishirikana na  Jumuiya Wanasheria Wanawake Zanzibar  (ZAFELA) na Jumiya ya Utetezi wa Jinsia na Mazingira Pemba (PEGAO) kupitia  udhamini wa Ubalozi wa  Norway nchini, kinatekeleza kwa pamoja mradi wa kuwainua wanawake  katika uongozi na haki zao za  kidemokrasia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top