Waandishi wa habari sitini (60) visiwani Zanzibar wameombwa kuboresha kazi wanazozifanya juu ya mradi wa uhamasishaji wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi (SWILL) ili kazi hizo ziweze kuleta mabadiliko chanya kwa jamii.
Mapema akifungua mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wa kuandika habari za uchambuzi juu ya ushiriki wa wanawake katika nafasi mbali mbali za uongozi waandishi wa habari sitini (60) wa Zanzibar, Mkurugenzi mtendaji wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa Zanzibar Dr. Mzuri Issa, amesema licha ya mafunzo pamoja na semina mbali mbali wanazozifanya bado jamii inakabiliwa na dhana potofu juu ya nadharia ya wanawake na uongozi, hivyo basi amewaomba waandishi hao kuboresha zaidi kazi zao ili ziweze kufikia malengo ya mradi huo.

Aidha
amesema wingi wa majukumu ya kifamilia ni miongoni mwa sababu zinazopelekea
wanawake wengi kushindwa kugombea nafasi za uongozi kwani hutumia muda mwingi
katika utekelezaji wa majukumu hayo.
“Kuna
sababu nyingi sana zinazopelekea wanawake wengi kutokufanikiwa kugombea nafasi
mbali mbali za uongozi lakini miongoni mwa sababu hizo ni imani potofu kwa
baadhi ya wanajamii juu ya mwanamke kujiingiza katika siasa pamoja na wingi wa
majukumu ya kifamilia” Dr. Mzuri
Kwa
upande wake mratibu wa Tamwa Pemba Bi. Fathiya Mussa Said, amesema lengo la
mafunzo hayo ni kuwapiga msasa waandishi wa habari kuweza kuandika habari za
uchambuzi ambazo zitaweza kuishawishi jamii pamoja na mamlaka mbali mbali
kuweza kubadili muelekeo na mitazamo kuhusu wanawake na ushiriki wake katika
siasa na upatikanaji wa demokrasia kataika uongozi.
“Kwahivyo
waandishi watakapo pata mafunzo haya
wataweza kutumia vyombo vyao katika kuandika habari mbali mbali za
uchambuzi, habari ambazo zitakuwa zina impact na data mbali mbali
zinazoonesha mafanikio na
changamoto za wanawake katika kugombania
nafasi za uongozi” Bi. Fathiya
Akiwasilisha
mada ya JINSIA na UONGOZI mwandishi wa habari kutoka
gazeti la Zanzibar Leo na Blogi ya Pembatoday Haji Nassor Mohammed, amewasisitiza
waandishi hao kuzidisha jitihada na ubinifu katika kuandika habari ambazo
zitaweza kubadili mitazamo hasi kwa wanajamii ili kuhakikisha usawa wa kijinsia
katika uongozi unapatikana
“Kwa mfano tumeona hapa katika sifa zote saba hakuna sifa ambayo imemtaja mwanamme hii ina maana kuwa suala la uongozi ni haki ya wanaume na wanawake, kwahivyo tunapoandika habari zetu tunapaswa kutoa elimu hii kwa jamii” Alisisitiza

Akitoa maelekezo juu ya namna ya kutengeneza vipindi bora vya radio na televisheni afisa habari na mawasiliano Tamwa Pemba Gaspery Charles, amesema mafunzo hayo ya siku tatu ni kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika kazi mbali mbali za waandishi wa habari juu ya mradi huo wa SWILL ikiwemo kukosekana kwa ubora wa sauti kwenye vipindi, ufuatiliaji mdogo, kukosekana kwa takwimu, uchache wa vyanzo vya habari, kukosekana kwa usawa wa kijinsia pamoja na uongezaji wa taarifa zisizo sahihi katika vipindi.
Amewaomba
waandishi wa vyombo hivyo kuandaa muongozo mzuri wa vipindi wanavyoandaa ikiwemo
kuwa na elimu ya wanawake na uongozi pamoja kufanya tafiti ili kuandaa vipindi
na makala zenye maudhui bora.
Akichangia
mada mwandishi kutoka shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Mchanga Haroub,
amesema moja miongoni mwa changamoto zinazowakabili waandishi habari juu ya
uandaaji wa vipindi hivyo ni ukosefu wa vitendea kazi vya uhakika pamoja na mazingira
yasiyo rafiki kikazi.
“Kwa
mfano unamkuta mwandishi ana idea mzuri yakufanya lakini akiangalia hana
vitendea kazi kwa mfano camera yenmye uwezo mzuri, usafiri au nauli kwa ajili
ya kutafuta sources, sasa kwakweli katika mazingira kama hayo ni vigumu kupata
makala bora” Mchanga Haroub
Nae
mwandishi kutoka blogi ya Full Shangwe Masanja MAbula, amesema kutokufahamu
lengo la uandaaji wa vipindi hivyo, kutokujituma pamoja na kutokuwa na ubunifu
kwa waandishi wengi wa habari kuna changia kwa kiasi kikubwa kuandaa vipindi
ambavyo havina ubora.
Nao
waandishi hao wameahidi kuyafanyia kazi mafunzo hayo ili kuzalisha vipindi
ambavyo vitakuwa na ubora vitakavyoleta mabadiliko chanya katika jamii.
Mafunzo
hayo ya siku 3 juu ya mradi wa uhamasishaji wanawake kushiriki katika nafasi za
uongozi (SWILL) yanajumisha waandishi sitini (60) ambapo ishirini (20) kutoka
Pemba na arobaini (40) kutoka Unguja na kuandaliwa na chama cha waandishi wa
habari wanawake Tamwa Znz, jumuiya ya Utetezi wa Mazingira na Jinsia Pemba
(PEGAO) jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar (ZAFELA) kwa ufadhili wa UbALOZI
WA Norway Tanzania.
Mafunzo
hayo ya siku 3 yameanza rasmi July 20, 2022 na kutarajiwa kukamilika July 23,
2022.