UKATILI; MUME AMUUA MKEWE KWA KUMNYONGA KISA MAPENZI.

0

 MWALIMU wa Shule ya Sekondari Tanga, Emmanuel Jerome (32), anadaiwa kumnyonga mke wake, Lucy Nshoma (34, katika nyumba ya kulala wageni mkoani Rukwa, kisha na yeye kujinyonga kwa kutumia kamba juu ya mti siku moja baadaye mkoani Katavi.


Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame amesema marehemu ni mkazi wa Tanga na chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi.

Kamanda Makame amesema marehemu Jerome alikua na mgogoro na mke wake, ambapo alimtuhumu kutoka kimapenzi na wanaume wengine.

Alisema Jerome na mkewe walipanga safari kuelekea mkoani Rukwa, ambapo ni nyumbani kwao marehemu mke wake na walifikia nyumba ya kulala wageni Julai 26, 2022, ndipo usiku alipochukua uamuzi wa kumnyonga mkewe.

Kamanda Makame alisema baada ya kumnyonga katika nyumba hiyo ya wageni, aliacha ujumbe wa maandishi kwa ndugu wa mke wake uliosomeka: "Nisameheni kwa yaliyotokea".

Alieleza kuwa baada ya kufanya tukio hilo mkoani Rukwa alikimbilia mkoani Katavi na Julai 27,2022 usiku, eneo la mtaa wa Ilembo, Manispaa ya Mpanda, alichukua uamuzi wa kujinyonga na walikuta mwili wake ukiwa unaning’inia kwenye kamba.

TAZAMA VIDEO HII YA WALIOKOSA UTEUZI WA UKUU WA MKOA.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top