VIDEO:DKT.GWAJIMA: WANA TAA JIUNGENI SMAUJATA TUOKOE WATOTO WANAKATILIWA HIVI

0

 Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,  Dkt Dorothy Gwajima amewataka Wanachama wa Chama cha Wahasibu Tanzania (Tanzania Association of Accountants-TAA) kuwa mstari wa mbele na kujiunga na Kampeni Huru ya kupinga Ukatili ndani ya Jamii ya SMAUJATA.


Dkt. Gwajima ameyasema hayo wakati akifunga mkutano wa 38 wa wanachama hao uliofanyika Jijini Dar es Salaam kwa siku mbili Julai 21 na 22, 2022,

Dkt. Gwajima alisema kila kundi katika jamii linapaswa kuchukua hatua dhidi ya vitendo  vya ukatili wa kijinsia na amewaasa wanataaluma hao kupambana na wimbi la Ukatili uliokithiri ndani ya jamii hivyo suluhu pekee ya kukabiliana nayo ni kwa kila mwanajamii kuona na kutambua hatari iliyopo na kuchukua hatua.

"Hatari ya watoto kufanyiwa ukatili ni kubwa na iwapo kila mmoja kwa nafasi yake hatachukua hatua kwa wakati wa sasa hata uchumi tunaojenga hautakuwa na ufanisi kwenye maendeleo maana, kwa kuwa utakuwa unatumika kwenye kuponya majeraha na vidonda vya manusura wa ukatili." alisema Dkt. Gwajima.

Ameongeza kuwa kwa miaka miwili iliyopita Watoto 27,369 walifanyiwa vitendo vya ukatili wa aina mbalimbali (sawa na wastani wa 1140 kila mwezi). Aidha, kwa mwaka 2021 waliobakwa walikuwa 5899 sawa na wastani wa 491 kwa mwezi na waliolawitiwa ni 1114 sawa na wastani wa 93 kwa mwezi. Aidha, ukatili huu ulifanyika kwa 60% kwenye familia wanakoishi watoto huku 40% ukitokea shuleni.

Akimkaribisha Waziri kufunga Mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula  aliwaambia wanataaluma hao kuwa tatizo la Ukatili wa kiuchumi bado lipo na linachagizwa na watu kuchukua mikopo bila ya kuwa na maarifa ya uendeshaji biashara hivyo kuutumia vibaya Mikopo.

Pia Dkt. Chaula aliwataka Wanataaluma hao kuandaa Mafunzo yatakayotoa tija ya mikopo kwa Wajasiriamali hususan wale wanaochukua kwenye Halmashauri mikopo ya asilimia 10.

Akizungumza muda mfupi kabla ya ufungaji wa Kikao hicho Katibu Tawala Mkoa wa Tabora...JINA  alisema zaidi ya Bil. 2 kwa upande wa mkoa wa Tabora hazikurejeshwa hali inayodidimiza jitihada za kuwakomboa wananchi.

"Shabaha ya Serikali dhidi ya Mikopo hii ni njema ikiwepo kuongeza walipa Kodi lakini kama Mikopo hii hairudishwi athari yake ni kuzidi kudidimia kwa uchumi, hivyo niombe mtumie taaluma yenu ya Uhasibu kuweza kuwajengea uwezo wajasiriamali kwa kuandaa vitabu vya kuwaelimisha" alisema JINA

Mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na waasisi wa Chama hicho uliwatunukia tuzo za kutambua mchango wao katika Chama hicho, ambapo Bibi. Happiness Nkya alitunukiwa mmoja ya tuzo hizo huku akishukuru na kuahidi kuwa Balozi wa kupambana na Ukatili.

TAZAMA VIDEO HII YA WAZIRI GWAJIMA AKITANGAZA TAKWIMU ZA UKATILI.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top