VIJANA WANNE WATUHUMIWA KUMBAKA MWANAFUNZI WA UUGUZI

0

 Polisi Mkoani Kigoma wanawashikilia Watuhumiwa watatu kwa tuhuma za kumbaka Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 19 Mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Tanga mwaka wa kwanza ambaye inaelezwa alibakwa kwa nguvu na Vijana wanne.

PICHA KUTOKA MAKTABA

Kamanda wa Polisi Kigoma Ramadhani Kingai amesema Mhanga alikamatwa kwa nguvu na kuingizwa ndani kisha kubakwa huku vijana hao wakifungulia redio kwa sauti kubwa.

"Mmoja ya Watuhumiwa aitwaye Bakari Hassani alimlagai msichana huyo kwa kuazima simu na kwamba kuna mtu anataka kumpigia ndugu yake wakati huo alikuwa akisogelea makazi yake na alikula njama na wenzake wengine walivyokaribia kwenye nyumba ambayo anaishi binti huyo walimkamata binti huyo na hatimaye kumuingiza kwenye nyumba waliyomfanyia ubakaji huku wakiwa wamefungulia redio kwa sauti kubwa ili kelele za binti kuomba msaada zisisikike, walipomaliza walikimbia"amesema kamanda

RPC Kigoma amewataja Watuhumiwa waliofanya ubakaji huo katika eneo la Mrusi kata ya Heruchuni Wilayani Kasulu kuwa ni Julius Yolemino(24), Hemed miosho (24) na Bakari Hassani(21) na Mtuhumiwa wa nne ambaye anafahamika kwa sura na aliyebakwa na bado anasakwa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top