WACHUNGAJI WALIOASI EAGT WAPEWA MUDA WA KUOMBA MSAMAHA

0

Hatimaye mgogoro wa Kanisa la EAGT uliodumu kwa kipindi cha miaka sita umemalizika na hivyo kuondoa mgawanyiko uliokuwepo katika Kanisa kutokana na mgogoro huo huku wachungaji walioliasi Kanisa hilo wakipewa wa kuomba msamaha ili warejee kufanya kazi ya Mungu kanisani humo.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Kanisa hilo jijini Dodoma,Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Brown Mwakipesile amesema,mgogoro huo umemalizika baada ya maamuzi ya uongozi wa Msajili wa Jumuiya ya Kanisa hilo kutoa  barua yenye kumbukumbu Na.SA. 7183/PARTVI/50 ya  30 Juni 2022.

Amesema,barua hiyo ina maelezo ya kina jinsi Serikali ilivyofanya Uchunguzi wa kutosha na mwishowe ikabaini kwamba tuhuma zote walizotuhumiwa Viongozi Wakuu wa Kanisa la EAGT hazina msingi na wala Viongozi hao Wakuu hawahusiki kabisa na tuhuma zote walizotuhumiwa nazo.

Baadhi ya viongoiz wa Kanisa la EAGT Kanda ya Kati wakimsikiliza Askofu wa Kanisa hilo Dkt.Brown Mwakipesile

“Jambo ambalo limeipa ujasiri Serikali yetu kutangaza kwamba, mgogoro umekwisha na kutambua Viongozi   halali wa Kanisa la EAGT kwa sasa kwa kuorodhesha majina  yao  jambo ambalo limefuta kabisa mawazo potofu yaliyokuwa yanaenezwa  kwamba kuna EAGT mbili.”amesema Askofu Mwakipesile

Kufuatia hatua hiyo , ametaja viongozi halali wa Kanisa hilo kuwa ni Askofu Mkuu Dkt. Brown  Mwakipesile, Makamu Askofu Mkuu Dkt. Joshua  Wawa,Katibu Mkuu Dkt. Leonard  Mwizarubi,Muhazini  Mkuu Dkt. Praygod  Mgonja na Mshauri Mkuu Dkt. Livingstone Dennes

“Mgogoro wa Kanisa ulitokana na aliyekuwa Makamu Askofu Mkuu wa kanisa letu  John Stephene Mahene kupinga kuondolewa madarakani kwa sababu za kukiuka miongozo ya imani ya kanisa letu ambapo alidai kuondolewa kwa sababu za kuhoji ubadhilifu wa fedha na mali za kanisa uliofanywa na viongozi wa kanisa.”alieleza chanzo cha mgogoro huo

Askofu Mwakipesile amesema,kutokana na kumalizika kwa mgogo huo Kikao cha Baraza la Waangalizi wa Kanisa la EAGT kilichoketi Julai 12 mwaka huu kimetoa  miezi mitatu kwa Mchungaji yeyote atakayetaka kurejea baada ya mgogoro kumalizika, kwa kuandika barua ya kutambua kosa lake ndipo aweze kupokelewa.

Mchungaji yeyote atakayetaka kurejea baada ya mgogoro kumalizika,atapokelewa na ngazi husika kwa sharti la kuandika barua kwa Uongozi husika kwamba ametambua kosa lake na sasa anaomba msamaha na kwamba yuko tayari kutumika chini ya Uongozi halali wa Kanisa la EAGT.”amesema

Amfafanua kuwa mwisho wa kupokelewa ni 20 Octoba 2022 na mlango wa maombi hayo ya msamaha utakuwa umefungwa. SOMA ZAIDI>>

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top