WAHAMIAJI 69 WAKAMATWA NJOMBE,WAWILI WAFARIKI KATIKA AJALI

0

Na:Fadhili Lunath Njombe

Wahamiaji haramu wawili kati ya 69 ambao wanadaiwa kuwa raia wa Somalia na Ethiopia wamefariki dunia baada ya kupata ajali kwenye mteremko mpakani mwa kijiji cha Kidope na Ubiluko wilayani Makete mkoani Njombe. 

PICHA KUTOKA MAKTABA

Taarifa za awali zinadai kuwa ajali hiyo imetokea alfajiri ya kuamkia Julai 7,2022 ambapo baada ya kutokea ajali hiyo wengine walikuwa katika hali mbaya huku wengine waliokuwa wamepata ahueni walianza kukimbia baada ya kuona watu wanawasogelea

 

Mganga mkuu wa halamshauri ya wilaya ya Makete Dkt.Ligobeti Kalisa amethibitisha kutokea kwa vifo viwili vya wahamiaji hao haramu huku akidai kuwa walikuta wakiwa na hali ya kuchoka sana kutokana na njaa,uchovu pamoja na baridi kali

‘mpaka sasa vifo ni viwili,mahututi ni watatu ambao wamepelekwa hospitali ya Ikonda,wengine wanaendelea na matibabu hospitali ya Bulongwa na wale ambao wako vizuri kiafya baada ya huduma ya kwanza wamepelekwa kituo cha Polisi’ amesema Daktari

 

Kwa upande wake kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe amethibitisha kutokea kwa tukio la ajali pamoja na vifo viwili vya wahamiaji hao haramu.

‘ni kweli kunatukio hilo,taarifa za awali zinaonesha walikuwa wahamiaji 69,ambapo mpaka tunazungumza ni kwamba watu wawili wamefariki dunia,25 wapo kituo cha polisi,18 wapo hospitali ya Bulonga na 15 wapo hospitali ya wilaya ya Makete na watatu wapo hospitali ya Ikonda’ amesema Kaimu kamanda.

 

Awali Green ilizungumza na afisa mtendaji wa kijiji cha Kidope Bi.Salome Mwakipesile na afisa mtendaji wa kata ya Iniho Bi.Norio Bukuku walieleza hali waliyoiona katika eneo la tukio na hatua walizozichukua

‘Inavyoonesha huyo dereva alikuwa anakimbiza gari na hana uzoefu na hizi barabara za huku ukinga hivyo ndio wamedondoka’ amesema Bi Bukuku.

Mariana Katala ni mmoja wa wananchi wa kijiji cha Kidope waliofika katika eneo la tukio ameeleza kupitia tukio hilo wamejifunza mambo mengi namna ya kushiriki kikamilifu katika ulinzi shirikishi kwani walikuwa hawajawahi kushuhudia matukio hayo katika maeneo yao

‘Tulikuwa tunasikia tu kupitia vyombo vya habari kuwa kuna wahamiaji haramu leo ndio tumejifunza,lakini wananchi waliwaonea kama binadamu wenzetu walianza kuwaokoa na kuwapa chakula’
amesema mwananchi.

 

Hii ni mara ya Pili wahamiaji haramu kukamatwa katika wilaya ya Makete mkoa wa Njombe kwa mwaka 2022 hali inayoonesha huenda imekuwa njia ya baadhi yao kupita katika anjia hiyo.

 WANANCHI WAMUANGUKIA DC AONDOKE NA MCHAWI WA KIJIJI


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top