WAKULIMA WATAKIWA KUCHANGAMKIA SUMU YA NYUKI

0

 WAKULIMA wametakiwa kuchangamkia fursa ya zao jipya la sumu ya nyuki, ambayo inatumika kutengeneza dawa mbalimbali zikiwemo za mfumo wa hisia (nerves), maumivu makali ya viungo pamoja na kuchanganya kwenye vipodozi.

Watakiwa kuchangamkia sumu ya nyuki

Mbunifu wa mashine zinazotumika kuvuna sumu ya nyuki ambaye yupo chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Patrick Kitosi,amesema hayo alipokuwa akizungumza na HabariLeo katika maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Dar es Salaam jijini Dar es Salaam.

Kitosi amesema mbali na kutibu magonjwa hayo, hivi sasa sumu hiyo inafanyiwa utafiti juu ya uwezekano wa kutengeneza dawa ya kansa na kuongeza kinga mwilini kwa magonjwa kama ukimwi.

Amesema kwa kushirikiana na tume hiyo, wametengeneza mashine za kisasa  kwa ajili ya kusaidia wafugaji wa nyuki nchini kuvuna sumu hiyo ambayo ikivunwa inauzwa kwa kuwa ina matumizi  mbalimbali kwenye sekta ya afya.

Amesema utafiti huo ulianza mwaka 2017 na hivi sasa sumu hiyo ipo kwenye hatua ya bidhaa ambayo imeanza kuuzwa kwa wakulima.

“Mashine moja inakusanya sumu kuanzia gramu 0.6 mpaka 1.5 ndani ya nusu saa. Gramu moja ya sumu hiyo inauzwa kuanzia sh 50,000 hadi Sh 350,000 soko la nje kulingana na ubora wake kwani gharama inategemea viwango,” amesema.

ULIPITWA NA VIDEO HII,BASI BOFYA TU HAPA KUTAZAMA DAKIKA MOJA INATOSHA!


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top