WALEMAVU TUSIPOWAJALI TUTAWAPOTEZA KWA KUWATENGA NA HUDUMA ZA JAMII

0

Serikali na jamii imekumbushwa kufanya ujenzi wa miradi mbalimbali unaozingatia mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu ikiwemo sehemu ya kutolea huduma au kufanyia biashara ili kutojiona wanatengwa ndani ya jamii.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Udiakonia iliyo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania Dayosisi ya kusini kati Tandala wakati wa Mahafali ya kumi ya wanafunzi wa ushonaji katika Idara hiyo yaliyofanyika julai 8 ,2022.


Mkurugenzi Elikana Kitahenga pamoja na mambo mengine amesema ukiangalia majengo mengi yakutolea huduma ikiwemo Makanisa, shule, maduka ya biashara na majengo mengi ya kupata huduma yamekuwa hayazingatii miundo mbinu rafiki kwa watu wenye ulemavu.


Akisoma Risala mbele ya Mgeni rasmi Augenia Thomas Mtweve ambaye ni miongoni mwa waliohitimu mafunzo ya ushonaji katika Idara ya Udiakonia Tandala amesema walianza wanafunzi watano lakini waliohitimu ni watatu na wengine wameshindwa kuhitimu kutokana na sababu mbalimbali.


Akitoa hotuba Mgeni rasmi katika mahafali hayo ya Kumi Mchungaji Mstaafu Foni Sanga wa KKKT amewataka wanafunzi hao kujiendeleza zaidi baada ya kupata msingi wa ufundi katika Idara hiyo na wazazi wawasaidie mtaji wasiishie kwenda kuwa tegemezi tena katika familia.

Katika Hatua nyingine Idara ya Udiakonia Tandala imesema wanafunzi baada ya kuhitimu hupewa vifaa vya msingi ikiwemo vyerahani kwa ajili ya kuanzia kazi. 

Baadhi ya wazazi na walezi walioshiriki Mahafali hayo wamewataka wahitimu kwenda kuwa na nidhamu katika jamii na kufanya kazi kwa kujituma pamoja na kushukuru Idara hiyo kwa namna ainayoendelea kuisaidia jamii.


Idara ya Udiakonia imesema kuwa mara nyingi ambao wanapewa nafasi ya kupata mafunzo ya ushonaji au useremala katika idara hiyo ni wenye mahitaji maalumu wakiwemo wenye ulemavu wa aina tofauti.

TAZAMA VIDEO HII MKURUGENZI WA IDARA YA UDIAKONIA AKIWALILIA WALEMAVU.

 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top