WANAUME NJOMBE WATAKIWA KUACHA KUPEKUWA SIMU ZA WAKE ZAO!

0

Wananchi wa vijiji vya limage na igominyi wilayani Njombe mkoani Njombe wameliomba jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia kuwasaidia wanaume wanaonyanyaswa na wake zao kufuatia baadhi yao kufikia uamuzi wa kujinyonga kwa kuona aibu kueleza changamoto hiyo kwenye mamlaka ikiwemo ofisi za serikali za vijiji.

Wakizungumza mara baada ya mkutano na jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsi mkoa wa Njombe waliofika kutoa elimu ya ukatili katika vijiji hivyo wananchi hao wamesema kuwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanaume vimekuwa vikitendeka katika vijiji hivyo lakini wanaume wanavumilia kwa sababu wanaona aibu kuviripoti na wengine wanaamua kujinyonga.

Devotha thomas ni afisa mtendaji wa kata ya Yakobi wilayani Njombe amesema ni kweli vitendo hivyo vipo na kwamba wakati mwingine wanaume wamekimbiwa mpaka chumbani hali inayowafanya wanaume kujikuta katika wakati mgumu na kuamua kujidhuru kwa kujinyonga baadhi yao.


Akitoa elimu ya ukatili wa Kijinsia kwa wananchi hao Mkuu wa Dawati la Jinsia kutoka jeshi la Polisi Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la Polisi Wilfred Willa amewataka wanandoa kuacha kuchunguza simu za wenza wao kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kwamba huko ndiko kunapelekea kukutana na jumbe kutoka kwa wenza wa kando wa wanandoa wao na kufikia hatua ya kujichukulia sheria mkononi.

ZAIDI TAZAMA VIDEO HII KUTOKA KWA WANANCHI WA MAENEO HAYO.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top