WATU 4 WANUSURIKA KIFO KWA KULIPUKIWA NA SIMU NDANI YA BAJAJI

0

Watu wane wamenusurika kifo baada ya kutokea mlipuko mkubwa uliyosababishwa na simu ndani ya bajaji yenye nambari za usajili MC 567C JK-TVC katika barabara ya Njombe -Songea .


Akizungumzia tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mkasa wa betri kulipuka umeleta taharuki kwa abiria na kusababisha  dereva kuacha usukani na kisha chombo kuacha njia na kupinduka.

Issa amesema punde baada ya ajali hiyo kutokea askari wanaolinda bank moja mjini Njombe wakafika kufanya uokozi na kuwakuta abiria wakiwa wamejeruhiwa na kuamua kuwakimbiza hospitali.

Katika hatua nyingine Kamanda ameshangazwa na kitendo cha mmiliki wa bajaji kumfata mmiliki wa simu na kumtaka amlipe gharama za ukarabaji jambo ambalo ni ukosefu wa uungwana.

Mbali na mkasa wa ajali,Siku chache zilizopita liliibuka wimbila vibaka katika mtaa wa Joshoni na Mjimwema ambako kulitendeka matukio ya ubakaji,Uvunjaji na Uporaji ambapo anasema operesheni kamata vibaka imefanyika na kuwatia nguvuni wahusika wa mikasa hiyo.

Pamoja na Yote jeshi la polisi limetoa rai kwa makampuni ya simu kutengeneza bidhaa zenye ubora ili kulinda afya za watumiaji.
TAZAMA VIDEO HII YA AJALI YA BAJAJI KULIPUKA KWA SIMU.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top