WATU WAWILI WATUHUMIWA WA UJAMBAZI WAUAWA NA POLISI

0

Majambazi wawili wameuwawa mkoani Kigoma na mwingine kutoweka kusikojulikana baada ya majibizano ya risasi na jeshi la polisi wakati walipojaribu kuvamia soko la Kijiji cha Bukirilo lililopo wilayani Kakonko mkoani humo.

RPC Kigoma ACP Menradi Sindano

 Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma ACP Menradi Sindano amesema awali  majambazi hao walivamia soko la Kijiji hicho majira ya saa 1 usiku wakiwa na silaha mbalimbali ikiwemo bunduki aina ya AK47 waliyotumia kutishia wananchi kabla ya kuanza kupora mali zao.

Aidha kamanda Menrad ameongeza kuwa  jeshi la polisi kwa kukishirikiana na raia wema walifanikiwa kuwafurusha majambazi  hao ambapo katika majibizano ya risasi majambazi wawili wamuwawa na mmoja kutoweka kusikojulikana.

Pamoja na mafanikio hayo kamanda Menradi amewataka wakazi wa Kigoma kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama pindi wanapobaini viashiria vya uhalifu katika maeneo yao.

TAZAMA VIDEO HII JIFUNZE KUTUMIA FACEBOOK KUPATA PESA.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top