Wananchi mkoani Njombe wametakiwa Kuendelea Kuwaenzi Mashujaa Wote Waliopambana na Wakoloni kwa Maslahi ya Watanzania Wote.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Waziri Kindamba alipofika katika kaburi la mashujaa la Pamoja lilipo Kijiji cha Utengule kata ya Kifanya Mjini Njombe, sehemu walipozikwa Mashujaa Waliokuwa Wakipambana na Jeshi la Wakoloni ambao Waliuawa na Wajerumani kutokana na Kupinga Utawala wa Kikoloni.
Aidha Mkuu wa Mkoa amewataka Wananchi Hususani Vijana Kuwa Wazalendo kwa Taifa lao kwani Mashujaa Wanaokumbukwa Leo Walitanguiliza Uzalendo kwa Taifa.
Awali kabla ya Kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kuzungumza Wazee wa Kijiji cha Utengule akiwemo Zakalia Magehema wakatoa Historia Juu ya Mashujaa hao Waliozikwa katika Kaburi la Pamoja.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amewataka Wananchi wa Kijiji cha Utengule kuwa wakwanza kukilinda Kivutio Hicho Kwani kinaweza kuwa chanzo cha Mapato katika serikali yao.
TAZAMA VIDEO HII YA WAZIRI KINDAMBA AKIONGEA NA WANANCHI.