Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Alhaj Othman Masoud Othman, leo Julai 31, 2022 amejumuika na Viongozi na Waumini mbalimbali wa Kiislamu, wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Alhaj Dkt. Husein Ali Mwinyi, katika Kongamano maalum la Kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1444 Hijria.
Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar, na kubeba Mada ya "Mafunzo ya Hijra kwa Waislamu", linafanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar, Msikiti uliopo Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Kulia ni Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mhe. Othman Massoud Othman na kushoto ni Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Kitengo cha Habari
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Julai 31, 2022.