AJALI NYINGINE YATOKEA SINGIDA YAKATISHA MAISHA YA WATU 5

0

Basi la Tanzanite lililopata ajali

Idadi ya vifo vilivyotokana na ajali ya basi la kampuni ya Tanzanite imeongezeka kutoka vifo vinne hadi vitano kufikia agosti 18,2022. 

Basi hilo lilipata ajali  Agosti 17, 2022, katika Kijiji cha Mbwasa wilayani Manyoni mkoani Singida wakati likitoka jijini Mwanza kuelekea Dar es Salaam.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida ACP. Stella Mutabihirwa, mapema hii leo na kusema gari hilo lilikuwa kwenye mwendo mkali hali iliyopelekea dereva kushindwa kulimudu na ndipo tairi la upande wa kulia lilipopasuka na basi kwenda kugonga tuta lililokuwepo pembezoni mwa barabara.

Kamanda Mutabihirwa, amesema kwamba katika ajali hiyo jumla ya watu 15 wamejeruhiwa katika ajali hiyo na kusema bado madereva wamekuwa wakiendesha kwa mwendo wa hatari bila kuchukua tahadhari, na kuwasihi madereva wafuate sheria za barabarani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top