Mtu mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria, aina ya Nissan Murano kugongana uso kwa uso na lori la kusafirishia mafuta, mali ya Kampuni ya Asas, tukio lililotokea alfajiri ya leo, majira ya saa 11 alfajiri katika eneo la Chimbuya mkoani Songwe katika Barabara Kuu ya Tanzania na Zambia.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Rashid Ngonyani amemtaja aliyefariki dunia kuwa ni Stanley Chengula, mkazi wa Tunduma ambaye alifariki papohapo, huku majeruhi akitajwa kwa jina la Flora Daniel mwenye umri wa miaka 22 ambaye naye ni mkazi wa Tunduma.
UMESOMA HII KUTOKA MAGAZETINI LEO NI AGOSTI 12,2022 SOMA KURASA ZA MBELE NA NYUMA
Kamanda Ngonyani amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori ambaye alihama upande wake na kwenda upande wa pili na kusababisha magari hayo yagongane uso kwa uso na kuongeza kuwa gari dogo lilikuwa likisafiri kutrokea Dar es Salaam kuelekea Tunduma huku lori likisafiri kutokea Tunduma.