ALIYETIKISA KIJIJI KWA UHALIFU AYEYUKA GHAFLA

0

Mikakati na mbinu za Siri walizojiwekea wananchi wa kijiji cha Kisinga wilayani Makete mkoani Njombe imetaja kuzaa Matunda katika kukabiliana na Wahalifu kijijini Hapo.

Mwenyekiti Wa kijiji

Mawazo Chaula ni Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji hicho amesema hali ya amani imerejea kutokana na kutokuwepo kwa matukio mbali mbali ambayo yanatajwa kuwa yalikuwa yakifanywa na mmoja wa wanakijiji hicho ambaye inadaiwa kuwa ametokomea kusikojulikana.

Chaula amesema wanaendelea kusimamia mikakati yao kwa ushirikiano wa viongozi na wananchi  ili kuhakikisha kuwa matatizo yaliyojitokeza kipindi cha nyuma hayajitokezi siku za mbeleni huku akitaja manufaa ya ulinzi shirikishi kuwa Umesaidia kuimarisha mapambano dhidi ya uhalifu.

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho akiwemo Demetrius Msigwa na Samsoni Chaula wamesema kurejea kwa hali ya usalama kijini hapo kumesaidia wananchi kuendelea na majukumu yao ya kila siku hali iliyotokana na Mbinu walizojiwekea katika kuleta amani kijijini hapo huku akisema sasa wako makini kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi wakikutana na changamoto ya aina yoyote.

Hata hivyo wananchi hao wameongeza kuwa yeyote atakayejaribu kuvuruga amani iliyopo watahakikisha sheria inachukua mkondo wake huku wakitoa wito kwa vijana kufanya kazi halali na kuepukana na vitendo vya uhalifu katika jamii.

Kabla ya hapo kijijini hapo kuliripotiwa uwepo wa mmoja wa wananchi aliyekuwa akiiba na kupora Mali za wananchi wengine nyakati za usiku jambo lililowalazimu wananchi hao kuandaa mikakati na mbinu  za Siri katika kukabiliana na Hali hiyo ambapo mpaka sasa inadaiwa kuwa mtuhumiwa wa matukio hayo ametokomea kusikojulikana baada ya maamuzi hayo ya wananchi wa kijiji hicho.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top