Askari wa kikosi Maalum Cha kuzuia magendo Zanzibar 'KMKM' aliyefahamika Kwa jina la Shaabani Mohammed Salum 33, amekutwa amefariki huko Machomanne Pemba akiwa amezungukwa na damu nyingi sehemu za kichwani.
Akitoa ufafanuzi juu ya marehemu huyo Daktari Dhamana wa hospital ya Chake Chake Abraham Said Msellem, amesema 21, 2022 majira ya saa 3:30 za asubuhi, ambapo amesema chanzo cha marehemu kupoteza Maisha ni baada ya kupata jeraha Kali eneo la upande wa kushoto wa kichwa ambalo lilipelekea fuju lake la kichwa kuharibika vibaya
"Majira ya saa 3:30 za asubuhi tulipata taarifa kuletewa mwili wa marehemu ambao unatambulikana kuwa ni askari wa kikosi Maalum Cha kuzuia magendo Zanzibar 'KMKM' Kwa jina la Shaabani Mohammed Salum mwenye umri wa miaka 33 na Kwa taarifa za awali marehemu amekutwa amefariki huku akiwa amezungukwa na damu nyingi maeneo ya kichwani, uchunguzi wa kitaalamu na wa mwanzo ulibaini Chanzo cha kifo Cha marehemu kumetokana na kuchomwa na kitu chenye ncha Kali ambacho kiliharibu kabisa fuvu la kichwa upande wa kushoto" alisema
Mwandishi wa Mawio alimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba kamishna msaidizi wa Polisi Abdalla Hussein Mussa, ambapo amesema bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa rasmi kwa vyombo vya Habari uchunguzi utakapo kamilika.
Chanzo: Mawio