ASKOFU MABUSHI AWATAKA WAZAZI KUACHA TABIA YA KUWAFUGA WATOTO BALI WAWALEE

0

 

WAZAZI na walezi wa manispaa ya Shinyanga wameaswa kuachana na tabia ya kuwafunga watoto kama wanyama bali wawe  wanawalea kwenye kutazama malezi zaidi  wawapo  majumbani.

Hayo yamesemwa  tarehe 21/08/2022 na skofu  David Mabushi wa   Kanisa la International Evangelical Assemblies of God Tanzania,lililopo  manispaa ya Shinyanga katika ibada ya jumapili,wakati akitoa mahubiri kwa  maandalizi ya wiki  ya watoto kwa kanisa hilo.

Mabushi  amesema wazazi na walezi wamekuwa na tabia ya kuwafanya watoto kama mifugo na kutowalea kwa msingi bora ya kidini na malezi  yaliyo muhimu ya jamii  matokeyo yake wamejikita  kufuatilia chakula na malazi  tu .

Mabushi  amesema  wazazi hawana muda na watoto na badaye kuwalaumu kuwa kizazi cha siku hizi kina shida,jukumun la wazazi kufatikia mwenendo wa watoto na kuwapa adhabu zinazostahili ili waondokane na ujinga na matendo maovu yasiyofa kwa Mungu na jamii.

Suzani Mabushi  amesema mikoa ya kanda ya ziwa baadhi ya   wazazi na walezi  wanamsukumo wa kupeleka watoto shule  ukilinganisha na mikoa ya kasikazini  lakini kupata mafunzo ya dini wanaona sio lazima. .

"Watoto tukae nao wenyewe wajue hali ya mzazi ikoje  kwa mazingira yoyote  tusiwapeleke wakakaa hovyo ndugu wengine sio watu wazuri" anasema Mabushi.

Ngatale Peter muumini wa kanisa hilo  amesema kuwa  changamoto iliyopo kwa sasa  ya kuwalea watoto  hovyo ni jambo  linalosababisha   kuwepo na athari za  vitendo vya ukatili  ni vyema kuwakumbuka watoto katika malezi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top