AUAWA KWA KUCHOMWA KISU AKIGOMBANIA MREMBO MPYA WA BAA

0

 

Wakaazi wa kijiji cha Motosiet eneo la Cherang’any kaunti ya Trans Nzoia walisalia katika mshangao baada ya kijana wa miaka 20 kuchomwa kisu na rafiki yake kwenye eneo la kuuza chang’aa hadi kufa.

Katika kisa cha Jumanne, Agosti 23,2022 mwendo wa saa nne usiku, Kevin Sakwa Wandabwa alichomwa kisu kifuani nje ya nyumba ya mfanyabiashara maarufu wa chang'aa Gladys Kipsingori.

 Sakwa na mshukiwa ambaye bado hajakamatwa, inadaiwa walitofautiana kuhusu mrembo aliyeajiriwa na Kipsingori kuuza kinywaji hicho na wakati uo huo kuwatumbuiza walevi.


 "Ilitokea kwamba marehemu alimuona mmoja wa wasichana hao na kumwendea, lakini inaonekana rafiki yake mmoja alihisi wivu na kubishana naye katika ugomvi mkali," Chifu wa eneo Isaac Kichwen aliambia Nation.

Katika makabiliano hayo, mshukiwa alimchoma kisu Sakwa na kumwacha akivuja damu. Kamanda wa Polisi wa Kaunti hiyo, Jecinta Wesonga, alisema mrembo huyo aliyekuwa akipiganiwa alitoroka huku wanakijiji waliokuwa na hasira wakichoma moto nyumba yake.

 Polisi pia wanamsaka Kipsingori, ambaye alitoroka baada ya kisa hicho. Mwili wa Sakwa ulipelekwa katika mochwali ya hospitali ya Rufaa ya kaunti ya Kitale huku uchunguzi kuhusu tukio hilo ukiendelea.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top