BABA AJINYONGA SIKU CHACHE BAADA YA KUJARIBU KUJIUA KWA KUNYWA SUMU

0

Na Bonface Mwafulilwa

Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Ikonda wilaya ya Makete Mkoani Njombe amejinyonga usiku wa kuamkia leo huku baadhi ya ndugu zake wakieleza kuwa marehemu alikuwa anapitia wakati mgumu kipindi cha uhai wake.


Akizungumza na Green fm Mdogo wa Marehemu Aroni Mbilinyi ameelezea namna alivyozipokea taarifa za kifo cha kaka yake.

'Kama ambavyo waandishi wa habari mlisikia huko nyuma kwamba alijaribu kujiua kwa kunywa sumu,tulisikitika sana tulimshauri mimi kama mdogo wake nilimshauri sana lakini mara hii ameamua kujinyonga tumempoteza' amesema mdogo wa marehemu.

Akizungumza na Green Fm kwa njia ya simu kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema marehemu alijinyonga shambani kwake lakini uchunguzi zaidi unaendelea.

'Mimi nina wito kwa wananchi hasa wa wilaya ya Makete endapo mtu ana taharuki ya aina yoyote au sintofahamu inayohusiana na familia au yeye mwenyewe asisite kuwaeleza watu wengi ili wamashauri,huyo aliyejinyonga ana miaka 47 na nyuma yake kuna watu waliokuwa wanamtegemea' amesema Kamanda Issa

Aidha Kamanda Issa ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Njombe kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwa kujinyonga kwani wanapofanya uamuzi kama huo wanawaacha wategemezi katika wakati mgumu.

TAZAMA VIDEO HII YA ORODHA YA WAKUU WA MIKOA WALIOTEULIWA NA SAMIA


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top