BABA ATEMBEZEWA KICHAPO BAADA YA KUKAMATWA AKIMBAKA MWANAFUNZI

0

 Mzee anayekadiliwa umri wa Miaka 59 amefumaniwa na wananchi wa mtaa wa Masekelo katika Manispaa ya Shinyanga ametembezewa kichapo na wananchi wenye hasira kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita.

Picha kutoka Maktaba


Mwenyekiti wa mtaa wa Masekelo kata ya Masekelo, Elias Mminda amesema tukio hilo limetokea Agosti 5,2022 majira ya saa kumi na mbili jioni.

Mminda ameeleza namna alivyopokea taarifa za tukio hilo ambapo amesema baada ya kufika katika eneo hilo alikuta wananchi wakimshambulia mtuhumiwa huyo.

“Majira ya saa kumi na mbili nilipigiwa simu nilikuwa nyumbani kwamba kuna binti amebakwa lakini sasa nina taarifa naye toka siku nyingi kuwa huyu mzee ana tabia za kuchezea wanafunzi, baada ya kufika hapa nimekuta wananchi wamemkamata baadaye sasa nikawapigia polisi ndiyo wamekuja kumchukua”,amesema.

“Wananchi wamemkuta akiwa na na mwanafunzi ndani nyumbani kwake maana huyu mzee anaishi peke yake tu, wazazi wa mtoto wamesema walikuwa na taarifa toka siku nyingi kuwa huyo mtoto huwa anaenda kwa kwa huyo mzee na walikuwa wakitafuta mbinu za kumpata leo ndiyo wamefanikiwa lakini binti nimemuulizia amekiri kuwa ni kweli huwa anakuja mara kwa mara kwa huyo mzee na amesema wameshafanya naye mapenzi mara nyingi tu”,amesema Mwenyekiti wa mtaa Elias

Kwa upande wao baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo wakati wakizungumza na Misalaba Blog wameiomba serikali kupitia jeshi la Polisi linalohusika kulinda usalama wa raia kuwachukulia hatua watu hao wanaoharibu ndoto za wanafunzi.

TAZAMA VIDEO YA BABA AKITEMBEZEWA KICHAPO KWA KUMBAKA MTOTO
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top