BATISTA AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KUMPA MWANAFUNZI MIMBA IRINGA

0

 Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha miaka 30 Batista Ngwale (27) kwa kukutwa na hatia ya kumpa mimba Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18 ambaye alikuwa akisoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kibena iliyopo Iringa vijijini.


Batista alikuwa akijishughulisha na kazi ya kinyozi ambapo ameiomba Mahakama kumpunguzia adhabu kwasababu ana Ndugu watatu na Mtoto mmoja ambaye anasoma Shule ya awali ambao wote wanamtegemea, maelezo ya Mahakama yanaeleza kuwa Kijana na Binti walifanya mapenzi mara mbili vichakani huku Kijana akijua dhahiri kwamba Binti huyo ni Mwanafunzi.

Kesi hiyo ilikuwa na Mashahidi sita akiwemo Daktari wa kituo cha afya cha Ifunda ambapo Binti alipelekwa kufanyiwa uchunguzi na kugundulika ana ujauzito wa wiki nne, Shahidi wa tatu ni Binti ambaye ameiambia Mahakama kuwa walianza mahusiano na Batista Mwezi May na walijamiana Mwezi June na baada ya mwezi mmoja alijihisi mjamzito na alimtaarifu Mhusika na akamshauri watoe lakini Binti hakutaka kutoa mimba hiyo na siku alipofika Mahakamani kutoa ushahidi alikuwa ni mjamzito.

Kesi hiyo imesimamiwa na Mawakili wa Serikali Radhia Njovu,Simon Nashon pamoja na Reuben Lubango ambapo waliomba mahakama kutoa adhabu kali kwa sababu kitendo hicho cha kufanya mapenzi vichakani kinamfedhehesha Mwanamke, akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa amesema kwa kuzingatia athari za kukatisha masomo ya Binti huyo na kumpa ujauzito,Mahakama imemkuta na hatia na imempa kifungo cha miaka 30 huku akipewa nafasi ya kukata rufaa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top