BUTIKU; VIJANA INGIENI SHAMBANI MLIKOMBOE TAIFA

0

 Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku, amewataka vijana nchini kujikita katika kilimo sambamba na kuwa dhamira na uvumilivu katika safari ya kulikomboa taifa kupitia sekta hiyo muhimu ikiwa ni pamoja na kutumia elimu waliyonayo katika kufanya kilimo cha kisasa.



Butiku ametoa rai hiyo agosti 17 2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vijana katika Uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha kilimo kwa vijana iliyopewa jina la 'Vijana na Samia tunaijenga Tanzania' kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutoa Bilioni 954 kwa ajili ya mapinduzi ya kilimo kwa kuwalenga vijana.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kampeni hiyo, Frank Festo amesema lengo la kampeni hiyo ni Kumuunga mkono Rais Samia, Katika juhudi za kunyanyua uchumi wa mtanzania kupitia Kilimo ambapo takribani bilioni tatu wanatarajiwa kukusanywa, watakaounda vikundi vitakavyotambulika na Brela ili kukuza mpango wa maendeleo ya taifa kwa miaka mitano na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top