CHIBALONZA ATEKWA NA PENZI LA BABU KIZEE WA MIAKA 88

0

Wanakwambia siku hizi kila mmoja anataka kumwagilia moyo wake bila kujali kinywaji gani atakitumia kumwagilia moyo wake ili uendelee kustawi lakini Mapenzi unaweza kusema ni miongoni mwa kinywaji bora zaidi kufanya moyo wako ustawi na kujawa na furaha.

Kauli za wahenga kuwa mapenzi hayana umri wengine wakisema Ng'ombe hazeeki maini imetokea huko nchini Congo baaada ya babu mwenye umri wa miaka 88 aitwaye Kasher Alphonse kuzama penzini kwa mtoto changa katika ulimwengu wa kupendwa mwenye umri wa miaka 22 aliyefahamika kwa jina la Chibalonza ambapo wanatofautiana umri wa miaka 66 na mumewe.

Kwa mujibu wa Makala fupi ya maisha ya wanandoa hao iliyoandaliwa na mtandao Afrimax English babu anasema wao wawili wanapendana bila kujalisha umri wao kutofautiana kwa kiwango kikubwa.


Kulingana na wapenzi hao ambao wamekuwa pamoja kwa miaka miwili sasa, walivutiwa na nyoyo zao na wala sio miaka na Alphonse alimuoa mke wake wa kwanza mwaka wa 1954 wakati alikuwa na umri wa miaka 24 na kujaliwa watoto saba pamoja.

Baada ya miongo kadhaa pamoja, mke wake wa ujana aliaga dunia kutokana na uzee, na kumuwacha babu huyo akiwa amevunjika moyo na mpweke kwani wanawe tayari walikuwa watu wazima na kuondoka nyumbani na kuendelea na maisha yao. 

Kwa kuzingatia umri wake wa uzee, Alphonse alihangaika kujifanyia mambo mengi, hivyo akatafuta mtu ambaye angemsaida kumwagilia moyo wake na bahati alikukutana na Chibalonza, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 20 lakini tayari kuwa mke wake.

"Hatujafunga ndoa rasmi lakini nimefanya naye harusi ya kitamaduni. Nilipeleka hata kreti ya bia na mbuzi aliye hai kwa familia yake," alisema.

 Mzee huyo alionyesha wasiwasi kuwa hajui jinsi watoto wake watakavyoishi na mama yao wa kambo iwapo atafariki dunia.

 Anajutia kuwa hana pesa za kununua kipande cha ardhi kwingine ili mke wake mchanga awe na makazi salama mbali na familia yake ya kwanza.

Watu wengi wanaojua kuhusu mapenzi huona kama ni ajabu kwa sababu watoto wote wa Alphonse ni wakubwa kuliko mama yao wa kambo, huku mwanawe wa kwanza akiwa na umri wa miaka 66, naye kitinda mimba ana umri wa miaka 50.

 Hivyo ndivyo unaweza sema mapenzi hayana mwenyewe hata maandiko yanasema ssi vyema mtu akae peke yake,kila la kheri kwa Mzee Alphonse kujipatia jiko,na kama una maoni zaidi unaweza kutuandikia hapo chini nasi tutayasoma na kufaanyia kazi kuhusu maudhui yetu na ungependa kusoma nini zaidi kupitia mtandao huu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top