Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha kupitia kikosi cha usalama Barabarani mkoa wa Arusha kimetoa elimu kwa madereva Zaidi ya mia moja (100) na kimewakumbusha madereva wa mabasi yaendayo mikoani kutii sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali kama sio kumaliza kabisha ajali za barabarani katika mkoa wa Arusha.
Hayo yamesemwa agosti 16 2022 na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi SP SOLOMON MWANGAMILO katika stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani na nchi Jirani ambapo amesema kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha kimejipanga vyema kudhibiti ajali katika mkoa wa Arusha.
Nao baadhi ya madereva wa mabasi yaendayo mikoani wamelishukuru Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha hususani kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha kuendelea kutoa elimu kwa madereva mara kwa mara ili kuwajengea uwezo na umahiri ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika.