HAJI MANARA:NILIENDA YANGA DAY KAMA MSHEREHESHAJI TU

0

HAJI Mnara,amesema kuwa kwenye tamasha la Wiki ya Mwananchi amehudhuria pale akiwa ni MC na sio msemaji wa Yanga.

Agosti 6,2022 katika kilele cha Wiki ya Mwananchi,Manara aliibuka na kufanya sapraizi kubwa kwa mashabiki na wanachama wa Yanga.

Ikumbukwe kwamba Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) ilitoa adhabu kwa Manara Julai 21 mwaka huu ilisema hatakiwi kujihusisha na masuala ya soka,hivyo hatakuwepo katika Tamasha la Mwananchi lakini aliibuka.

Manara aliingia uwanjani akisindikizwa na walinzi kisha akachukua jukumu la kutambulisha wachezaji na benchi la ufundi kisha akaaga akisema anaondoka kwani alialikwa kuwa mshereheshaji tu.

Baada ya utambulisho Yanga iliweza kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Vipers FC na ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 0-2 Vipers SC.

KISHERIA HILI LIKOJE! HEBU SOMA HII
Mdau wa soka  Julius Mtatiro ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru hakusita kutoa maoni yake hapo jana akiwa anafatilia Mwananchi Day ambapo gumzo mojawapo ni Haji Manara kuingia uwanjani na kutambulisha Wachezaji wakati amefungiwa kujihusisha na soka kwa miaka miwili.

DC Mtatiro ambaye ni Mfuatiliaji mkubwa wa soka alijibu kwenye comments baadhi ya Watu waliokuwa wakihoji uhalali wa Manara kuingia uwanjani na kusema kisheria hakuna kosa alilotenda Haji Manara.

“Kisheria hakuna kosa alilotenda, hapo uwanjani kumekuwa na mambo mawili, la kwanza ni sherehe ya Yanga inayosimamiwa na Yanga kama klabu“.

“Halafu kuna mechi ya kimataifa ya kirafiki kati ya Yanga na Vipers ambayo inasimamiwa na TFF, tukio alilosimamia Haji la kutambulisha Wachezaji na kusherehesha halimo kwenye masuala yanayosimamiwa na TFF, CAF au FIFA n.k ndiyo maana baada ya kusherehesha Haji ameondoka uwanjani ili kuendelea na kifungo alichopewa na TFF, nadhani sasa kisheria nimeeleweka” 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top