HAWA NDIO WACHEZAJI WALIOONDOKA SIMBA NA KUJIUNGA NA SINGIDA BIG STARS

0

 

Beki bora wa muda wote eneo la kati ndani ya Simba,kwa muda ambao alikuwa hapo  Pascal Wawa sasa atakuwa ni mali ya Singida Big Stars.


Ikukumbwe kwama Wawa alikuwa ni chaguo la kwanza kwa makocha ambao wamepita Simba ikiwa ni zama za Masoud Djuma,Patrick Aussems,Didier Gomes na zama za kocha wa makombe Pablo Franco alianza kuwekwa benchi.


Kwenye tamasha la Singida Big Day ambalo lilifanyika Uwanja wa Liti nyota huyo aliweza kutambulishwa pia.
 Kwa nyakati zake alizokuwa Simba alikuwa ni beki mwenye uwezo wa kupiga pasi ndefu na zenye uhakika akiwa sawa na Kelvin Yondan wa Geita Gold ambaye ni mzawa.


Mbali na Wawa pia Singida Big Stars imemtambulisha Meddie Kagere kuwa ni mali yao kwa msimu wa 2022/23 wakitokea Simba.


Pia Singida United iliweza kuwatambulisha wachezaji watatu wa Kibrazil,mmoja kutoka Zambia na wachezaji wengine ambao walikuwa na timu hiyo ndani ya Championship ikiwa ni Nicolas Gyan, Amis Tambwe,Juma Abdul na James Kotei.


Pia staa Said Ndemla naye ni mongoni mwa nyota wapya wa timu hiyo ambayo inatumia Uwanja wa Liti kwa mechi za nyumbani.


Kocha Mkuu ni Hans Pluijm alitangazwa na Nizar Khalfan atasaidiana na Mathias Lule kwenye upande wa makocha wasaidizi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top