HUYU NDIE MWALIMU ANAYEVUKA MTO KWA KUPIGA MBIZI ILI KUWAHI SHULENI

0

Simulizi ya mwalimu mkuu mmoja katika shule ya msingi nchini Ghana ni moja ya kutia matumaini sana baada ya kugundulika kwamba mwalimu huyo mkuu anapiga mbizi katika mto ili kuvuka na kuwahi shuleni kutoa huduma ya elimu kwa watoto.


Mwalimu huyo kwa jina Mensah Kwame analazimika kusafiri umbali wa kilomita kadhaa kutumia pikipiki yake iliyochakaa na ikiharibika hulazimika kuvua nguo kando ya mto na kupiga mbizi kuvuka ili kuwahi shuleni.

Inaelezwa kwamba, baada ya kusafiri kwa kilomita tisa, analazimika kujitosa mtoni kama samaki ili kuvuka na kisha kuendelea na safari iliyosalia ya kilomita tatu zaidi kufika shuleni, eneo ambalo linaonesha mazingira ya shule si rafiki. 

“Kama mwalimu katika eneo hili la mashambani, ninalazimika kuamka asubuhi sana. Hata ninapoondoka, familia yangu inabaki na wasiwasi kwa sababu njiani kuna mto. Hata hawana uhakika iwapo ninavyoweza kurudi nyumbani baada ya shule," Mwalimu Mensah Kwame alielezea.

Mwalimu Kwame amesema kwamba mara nyingi anapofika katika mto huwa hakuna mtu mwenye jahazi la kuwavusha upande wa pili, hivyo hulazimika kuvua nguo na kupiga mbizi mpaka upande wa pili, kuchukua jahazi na kurudi nalo upande wa kwanza kuchukua nguo zake na baadhi ya vitu vingine na kisha kuvuka tena kuendelea na safari kuelekea shuleni.

“Mara nyingi wakati tumefika kando ya mto, hakauna mashua ya kutuvusha upande wa pili, na kwa hiyo kama mwalimu inanibidi nivue nguo na kupiga mbizi upande wa pili kuleta mashua ili kuchukua vitu vyangu na kuvuka navyo tena,” Mwalimu huyo alisema.

Aidha, alisema kwamba walijaribu kuomba hifadhi karibu na eneo la shule ili kurahisisha usafirishaji wao ila ikashindikana kabisa na kwa hiyo inawabidi kusafiri kilomita kadhaa kila siku ili tu kuwafundisha wanafunzi.

Chanzo: Global publisher.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top